Piga Picha Shereheni, Wageni Wanunue
Papo Hapo kwa AI Ndani ya Sekunde 2!
Jukwaa maalum kwa ajili ya wapiga picha (cameramen) Tanzania. Pakia picha kutoka kwenye kamera yako, wageni wajipige selfie moja tu na kupata picha zao zote papo hapo (ukumbini, fukweni au sherehe yoyote). Wageni wanalipia kwa M-Pesa au Tigo Pesa, na pesa zote zinaingia moja kwa moja kwenye simu yako!
Wapi Unaweza Kuingiza Pesa Nyingi Papo Hapo na Kamera Yako?
Hauhitaji kusubiri sherehe za harusi pekee! Hapa kuna maeneo moto moto ambapo ukienda na kamera yako, watu wapo tayari kununua picha zao papo hapo:
Makanisani & Ibada Maalum
Ibada za Jumapili, Pasaka, Krismasi, kipaimara, ubatizo na harusi za kanisani. Waumini na familia wanapendeza sana. Piga picha zao nje ya kanisa, wanaskani QR yako, wanapiga selfie moja na kupakua picha zao papo hapo simuni kabla ya kuondoka!
Beach & Fukwe za Bahari
Coco Beach, Kigamboni, Mbudya, Bongoyo, Bagamoyo, Kawe, fukwe za Zanzibar na maziwani. Maelfu ya watu wanatoka kupumzika na familia au marafiki. Hawataki kusubiri siku kadhaa kutumiwa picha; wanataka picha zao kali hapo hapo ufukweni za kupost WhatsApp Status na Instagram mara moja!
Harusi, Send-off & Kitchen Party
Mlimani City, Serena Hotel, Diamond Jubilee na kumbi zote. Wageni 200 hadi 600 wamevaa suti na magauni ya kifahari. Weka vipeperushi au waonyeshe QR code ya tukio. Wageni wanajinunulia picha zao wenyewe bila wewe kupoteza muda kusambaza flash au kufuatilia watu!
Mahafali ya Vyuo & Shule
UDSM, CBE, IFM, IAA, MZUMBE, SAUT, DIT na mahafali ya shule za sekondari. Maelfu ya wahitimu wakiwa na majoho pamoja na wazazi na ndugu zao wenye furaha. Wanataka picha za ukumbusho papo hapo viwanjani kabla ya sherehe kuisha.
Viwanja vya Michezo, Marathons & Gyms
Marathon za Dar es Salaam, Kilimanjaro Marathon, mechi za mpira, matamasha ya riadha na mazoezi ya gym. Wakimbiaji na wanamichezo wanapenda sana picha zao wakiwa kwenye hatua za ushindi na medali zao!
Birthday Parties, Klabu & Matamasha
Viwanja vya burudani, sherehe za kuzaliwa na matamasha ya wasanii. Vijana na mashabiki wanataka picha zenye ubora wa kamera kubwa mara moja wakiwa bado wapo kwenye vibe la burudani.
Tazama Ni Pesa Ngapi Unaweza Kuingiza Simuni Mwako!
Weka idadi ya watu na bei unayotaka kuuza uone pesa inayotua mfukoni mwako:
Faida Kubwa kwa Studio & Mpiga Picha
Imeundwa kutatua changamoto halisi za biashara ya picha Tanzania na kukuongezea kipato.
Pesa ya Moja kwa Moja Simuni
Kila mgeni anaponunua picha, pesa inatua kwenye akaunti yako. Hakuna madeni, hakuna kusubiri mwezi uishe!
Ulinzi wa Kazi Yako (Watermark)
Hakuna anayeweza kuscreenshot wala kupakua picha ya wizi bure. Watermark inaondoka baada tu ya malipo kuthibitishwa.
Wewe Ndio Unayepanga Bei Yako
Una uhuru wa kuamua unauza picha kwa shilingi ngapi (mf. TZS 500, TZS 1,000 au TZS 2,000) kulingana na hadhira yako.
Hakuna Kuchambua kwa Mkono
AI inamtafutia kila mtu picha zake binafsi kwa sekunde 2 tu kwa kupiga selfie 1 tu popote walipo (fukweni au ukumbini)!
Mitandao Yote ya Simu Tanzania
Inakubali moja kwa moja Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Halopesa papo hapo.
Hakuna App ya Ku-install
Wageni hawalazimiki kupakua app yoyote; wanafanya kila kitu kupitia browser ya kawaida kwenye simu yao yoyote.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Kila kitu unachohitaji kufahamu kabla ya kuanza.
🔍 Je, Una Tukio Lililopo Tayari?
Weka Event ID kuingia moja kwa moja kwenye dashibodi ya mpiga picha au ukurasa wa mgeni.